BlokoRETO en Swahili


VIPI IKIWA UNAWEZA KUBADILISHA DUNA KWA  KUPIGANGOMA TU?

KIKUNDI CHA KIJAMII BLOKO DEL VALLE NI ZAIDI YA MUZIKI,ZAIDI YA NGUMA  ,NI NJIA YA KUBADILISHA DUNIA!

HII NI CHANGAMOTO MPYA KWA BLOKO….BILA MIPAKA!

Huu ni uzinduzi wa Bloko mpya-changamoto «Bila mipaka».tunahitaji kupata ngoma mia moja mpya ili kuongeza katika ngoma mia na ishirini  tulizo nazo kwa sasa.Hii itaturuhusu kufikia watu zaidi na kuwa kikundi kikubwa zaidi cha ungamano cha ngoma  ndani ya uropa.Kile  ambacho kilionekana kuwa ndoto sasa kimefanyika kuwa cha kweli.Hatua ambazo tumechukua zimechangia katika maendeleo ya madili na uhusiano wa kijamii mongoni mwa mamia ya watu. Kwanjia ya ngoma tuna uwezo wa kutia moyo watu kwa kuingiza ushirikiano ,kujieleza na ugunduzi wa kibinafsi.Tumeunda nafasi ya kuchunguza kwa ndani masuala kama uaminifu,Kujiheshimu na kukuza uhusiano kati ya watu binafsi,vikundi na jumuia nzima ambapo watu wanaweza kupata hali mpya nakuishi nje ya ndoto zao katika hali ambazo hazijafikiriwa hapo awali.

Watu wengi zaidi wanajiunga na sisi kila siku , watu binafsi na vikundi wanatujia wakitamani maono yetu ya muziki kama chombo cha mabadiliko ya kibinafsi na ya pamoja .

Ngoma sio ngoma tu,na kucheza ngoma ni zaidi ya kucheza ….

Ushirikiano wako,kuanzia mia moja tu, itageuzwa kuwa ngoma na kuongezwa kwenye nguvu ya ngoma za Bloko  ambayo unaweza kuiskia kila wakati ngoma zinapolia na zinapocheza…..kila mia itatumika katika kusaidia ungamano huu wa wapigaji ngoma katika harakati za kufikia watu zaidi hapa kwenye kisiwa cha Tenerife Spain na shule zetu za ngoma katika inchi ya Kenya na Cape verde, ….na kusaidiana kupanua upeo wetu na changamoto za mwaka ujao,kama vile kufanya kazi na makundi yasiojiweza huko Jodpur (India) na San Jose (Costa Rico) sisi tayari tuna jua kwamba tunaweza kubadilisha ulimwengu na kitu kidigo sana …..Utatusaidia kwa hii changamoto?

Fungua hii link kujiunga na changamoto ya Bloko «Bila mpaka”https://goo.gl/Nirp9v


 
A %d blogueros les gusta esto: